Tafuta Muda wa Kujichunguza Na Kujifahamu.

Posted by Apolinary Macha on 20:10 with No comments



Wengi wanapoamka asubuhi kuanza kujiandaa na shughuli zao mbalimbali. Mfano kama ni mwanafunzi anajiandaa kwenda shule na kama ni mfanyakazi naye anajiandaa kwenda kazini. Mzunguko huu huishia pale mtu anaporudi nyumbani, anapumzika labda kwa kutazama Television, au anasikiliza redio, au unaposhiriki maongezi mbalimbali na mwisho siku inaisha unapolala. Gurudumu hili litaendelea hapo kesho yake na kama siku ya kesho ni tofauti labda ni siku ya weekend basi kunakuwa na gurudumu lingine la mfumo wa kuifanya siku ipite.

Je unatenga muda wa kuweza kujitafakari? 

Wengi wanatumia siku yao kujituma, kufanya majukumu yao, kushirikiana na wengine n.k lakini ni wachache sana ambao hutumia muda fulani maalumu kwa lengo la kujitafakari. 

Inapaswa kutenga muda ambao utakuwa huru, hautaingiliwa na mtu katika mazungumzo ya muda mrefu, au hautapata usumbufu wowote. Muda huu utakuwa unajitafakari vyema. Unaweza ukawa unajitafakari kwa;
  • Kutafakari siku ilivyoenda/inavyoenda,
  • Kutumia nafasi kupumzisha akili,
  • Kujitafakari

Kujitafakari.

Kujitafakari ni kujiangalia kwa kina, kujitazama matendo yako yanavyoenda, kujitazama maneno yako na vitendo vyako vinavyoenda. Katika kujitafakari unaweza ukajitafakari jana ulikuwaje na leo umebadilikije. NI vyema kutumia kila siku kujirekebisha na kuondoa mizizi ya uovu inayokutawala. Kama wewe unafahamu kuwa udhaifu wako ni ulevi basi unajitafakari kwa kujiuliza "Kati ya jana na leo, je umejitahidi kujitawala?", na kama hujajitahidi utajiuliza ni kwanini, lazima ufahamu sababu. Na kama umejitahidi basi ni vyema kujipongeza na kujitahidi zaidi yapo kesho. Lengo ni kuhakikisha kila siku unajibadilisha. Unajibadilisha kwa kufuata mema na kuacha mabaya, pia unajibadilisha kuwa kuendeleza mema ambayo tayari umeyapanda. 

Tutafakari kuwa maisha ya hapa duniani ni machache sana, kulinganisha na maisha ya baadaye. Kama utaishi miaka 80 au zaidi bado hujafikia maisha ambayo yanaendelea baada hapo. Tafakari ni wangapi waliokufa miaka ya zamani, na muda gani umepita mpaka leo? Na kama bado wapo wapo wapi? Je wanaishije muda huu? Utaona maisha ni mafupi sana. 

Badala ya kupoteza muda kufanya majukumu, kujenga n.k wakati vyote hivi vinapita na tunaviacha hapa duniani tunapaswa kufahamu kuwa lengo la maisha ni kujitambua. Unapojitambua utabadilisha mabaya yote na kuhakikisha unajiweka imara katika matendo, mawazo na maneno sahihi. 

Huu ni wakati wako kujifunza na kujirekebisha sahihi, katika safari hii ya maisha ambayo haifahamiki itaisha lini. 

Asante.