Mambo ya Kujua Katika Kutimiza Ndoto Unayoipenda

Posted by Unknown on 18:11 with 2 comments
Mara nyingi katika kutimiza malengo yetu mwanzoni unaona ni vigumu kutimiza, kisha baada ya kujaribu unaanza kuona inawezekana kutimiza malengo. Baada ya kutimiza malengo utaona kumbe ilikuwa rahisi kutimiza malengo. 

Umewahi kutamani kutimiza malengo fulani kutokana na kupenda malengo hayo? Kuna wakati unaona kama ni vigumu kufikia pale unapopanga kufikia. Hii ni kawaida, hata wengi waliofika mbali nao kuna wakati waliona ni vigumu kufika walipofika leo. 

Katika kuweka jitihada kufikia malengo yetu, tunakutana na changamoto mbalimbali. Watu kuona kwamba hutoweza kufikia malengo yako, matatizo ya kifedha, mazoea ambayo yanaturudisha nyuma kimaendeleo, ugumu wa kupanga mipango yako na changamoto mbalimbali katika maisha. Lakini inashauriwa kufika mbali na kutokata tamaa kabisa. 

Kama upo katika safari ya kutimiza malengo yako na unapambana na changamoto mbalimbali kuna vitu vya kujifunza ambavyo vinaweza kusaidia. 




1. Hakuna aibu katika kufanya unachokipenda. 

Unapokuwa bado unajifunza ambacho unapenda hapo baadae kuwa mtaalam katika hicho kitu, unaweza kuona kama bado hujaweza na kujisikia vibaya kwa hilo. Fikiria ukifanikiwa kuwa mtaalam mzuri wa hicho kitu utajisikiaje? Hivyo badala ya kuwaza kuwa bado huwezi, jifunze kuwaza na kutambua kuwa ukifanikiwa kuweza unachokipanga utapata furaha zaidi na utazidi kuwa na ujasiri nacho. Enjoy kila sehemu ya safari, hata mwanzo wa safari ni mzuri. 

2. Vikwazo ni sehemu ya Safari

Kama nilivyoelekeza hapo mwanzo, kukutana na changamoto ni kawada katika maisha. Kila lengo na mpango unaotaka kutimiza unaweza kukutana na changamoto mbalimbali. Hii ni kwasababu changamoto ni sehemu ya safari ya maisha na malengo kwa ujumla. Ni vyema kutorudi nyuma au kukata tamaa. Changamoto zipo kutupima kama tupo imara, hivyo zichunguze changamoto kisha tafuta namna ya kuzikabili na endelea na safari bila kurudi nyuma au kukata tamaa. 

3. Jiwekee mazingira ya kuongeza Inspiration/msukumo.

Katika kutimiza malengo ambayo tunawaza na kuyapanga, kila siku jizoeshe kufanya kitu ambacho kinahusiana na mipango yako na kukupatia hamasa na msukumo wa kufikia mbali. Soma vitabu, andika malengo, tazama makala mbalimbali kama ni biashara, taaluma, kazi, n.k. Ni katika kuweka Subconscious mind kuwa sawa na malengo yako.