Upande wa pili wa kuwa “Single”

Posted by Apolinary Macha on 14:04 with No comments

Tunaposema upande wa pili, ina maana ya kuwa; ni upande ambao wengi hawautazami. Upande huo ni faida ya kuwa mpweke. Je kuna faida gani ya kuwa mpweke?


Wengi wana mtazamo mmoja kuhusiana na mtu aliye peke yake bila mahusiano yoyote. Wengi huona ni tatizo au jambo la ajabu. Wengine huona ni taabu na upweke. Leo katika sehemu ya mahusiano hatutaangalia mada zinazohusu watu wawili, leo tutatazama mada inayohusu mmoja. Mada ya leo ni kuangalia upande wa pili wa kuwa “Single” yaani kutokuwa na mahusiano.

Kwa walioachana na wapenzi wao, kwa ambao bado hawajaingia katika mahusiano, hivi sasa wanaweza kutumia nafasi hii kujifunza na kufahamu wanachoweza kufanya katika wakati huu wakiwa peke yao. Kwanza kabisa tutambue kuwa, huwezi kuishi na mtu kama hujui kuishi vyema wewe mwenyewe. Kuanza kujipenda vyema ni hatua ya kwanza kabla ya kumpenda mtu. Huwezi kumpenda mwenzako kama wewe mwenyewe hujipendi. Hivyo ni vyema kuanza kujua jinsi ya kuishi peke yako kabla ya kuishi na mwingine.

Kuwa Single kunakupa muda wa kuwa mwenyewe

Ukishaanza mahusiano utapata muda kidogo wa kuishi peke yako na kuwa peke yako kuliko awali. Ukiwa bado hujaanza kuwa na mahusiano ni muda wa kijuchunguza, kujitambua, na kuishi kiusahihi kwa kuifuata ‘True Nature’ yako. Ni wakati wa kujirekebisha na kujiweka sawa kabla ya kuwa na mtu. Ni vye kutumia muda huu kujitambua na kujiweka kiusahihi kwa ajili ya kuandaa mahusiano mazuri katika mapenzi na ndoa.

Ni wakati wa kujua nini cha muhimu

Kuwa Single ni muda wa kujichunguza na kutambua mambo ya muhimu na kuyazingatia zaidi. Unapokosa kitu ndipo utajua umuhimu wake, ni sawa na ukiwa Single ni wakati wa kufahamu vya muhimu unavyovikosa na kujifunza, pale wakati utakapofika utaheshimu wakati huo kwa sababu unajua maumivu ya kupoteza nafasi nzuri katika maisha.

Kuwa single haimaanishi hupendwi.

Huu ni wakati wa kujipenda kwanza, kujithamini na kujijali. Ni vyema kutoona hupendwi, kwa kuanza kujipenda mwenyewe. Ni vyema usikimbilie mahusiano na chunguza kwanza. Usikimbilie mahusiano kutokana na tamaa bali ingia kwenye mahusiano kama unaona kuna umuhimu na umempenda kwa dhati uliye nayo

Ni wakati wa kuamua sifa za unayetaka kuwa naye

Ukiwa Single, ni wakati wa kuamu ni tupi uwe naye na awe na sifa gani. Zingatia sifa za muhimu kwanza. Kumbuka kuna watu wapo kwenye mahusiano na hawawapendi kwa dhati wenza wao. Wengine unakuta inatokana na kuwa kuna sifa anazikosa kwa mwenza wake. Ukiwa Single unakuwa na uhuru wa kuamua unayemtaka aweje, ni sawa na bado una nafasi ya kuchagua kabla kujafanya maamuzi.

Ni wakati unaoweza kuutumia kufanya mambo ya maana

Haimaanishi walio katika mahusiano hawapati muda wa kufanya mambo ya maana, bali kwa wale ambao wapo wapweke na wanapoteza muda wao mwingi kusikitika, kujutia kutokana na mahusiano ya zamani na hivi sasa wanajiona wapweke baada ya kuachana; wanapaswa kutumia wakati huu wasiweke mawazo kwenye upweke bali watumia muda wao kufanya mambo ya maana. Jitume kazini, soma kwa bidii, jirekebishe tabia kama kuna tabia unapaswa kujirekebisha, ondoa uvivu na fanya mambo ya muhimu maishani. Usipoteze muda wako.

Ni wakati wa kujali familia na marafiki

Ukiwa single ni wakati mzuri wa kuwa karibu na marafiki na familia. Ongeza upendo kwao na uonyeshe kujali.

Kumbuka kila jambo lina upande Chanya. Hivyo tambua hali uliyo nayo na itumie kiusahihi. Ipo siku utafikia malengo yako kwa bidii yako. Usisikitike kwa kuwa mpweke bali tumia wakati huo kuwa “Positive”.