Jinsi Meditation inavyoweza Kubadili Furaha

Posted by Unknown on 11:40 with 1 comment
Jitambue Sasa
Meditation ni zoezi zuri la kuongeza furaha maishani.
Mojawapo kati ya faida kubwa katika meditation, ni kukupa umakini katika akili yako. Meditation imekuwa ikitumika kwa watu wenye stress na wenye matatizo ya kuwa na umakini. Ukiweza kuiweka akili katika tukio moja, au fikra moja, au hali moja, utaweza kuitawala akili yako vyema na kutokuwa mtumwa wa hali, hisia, mawazo, mazoea au mawazo hasi (negative thoughts). 

Katika kitendo cha kufanya meditation mara kwa mara, utajikuta umakini wako unabadilika. Hali yoyote inayojitokeza akilini na nje ya akili (katika mazingira yanayokuzunguka) nayo itabadilika na utaanza kuwa mtambuzi mzuri. Umakini utakusaidia kuwa na furaha wakati wote kwani utaanza kuwa na mazoea ya kuwaza mawazo chanya badala ya mawazo hasi. Hali yoyote ile mbaya utaiona kwa umakini na utakuwa unafanya maamuzi sahihi kwani una umakini mzuri katika kuona.

Umakini unaojifunza katika meditation unaweza kukusaidia vyema katika kufanya maamuzi, kushinda stress na msongo wa mawazo katika kipindi kigumu na kukusaidia kutazama hali za maisha kwa undani zaidi ya mtu wa kawaida aonavyo. Itabadili furaha yako na kuifanya izidi kuwa kubwa na ya kudumu kwa muda mrefu.