Majaribio ya Kisaikolojia Duniani Yaliyoweza Kusaidia Wanasaikolojia Kuelewa Zaidi Kuhusiana na Nature ya Akili ya Mwanadamu na Matendo yake.
Posted by Apolinary Macha on 10:00 with No comments
Mwanadamu anaweza akawa anahisi anaelewa mengi lakini kiuhalisia kuna mengine bado hatujayaelewa kuhusiana na sisi wenyewe katika kutambua nature ya asili ya mwanadamu. Akili ya mwanadamu mpaka leo ni sehemu ambayo haieleweki vyema. Katika saikilojia kuna baadhi ya tafiti ambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi fulani tuzidi kuelewa akili ya mwanadamu na matendo yake vyema na jinsi tunavyoitazama dunia inayotuzunguka. Lakini bado kuna mengi tunapaswa kuyafahamu zaidi.
Kuna baadhi ya tafiti zilizofanyika ambazo zinaweza kutusaidia kuelewa jinsi akili ya mwanadamu ifanyavyo kazi.
1. Stanford Prison Experiment.
Ni mojawapo ya tafiti kubwa ya kisaikolojia inayofahamika sana duniani katika kufahamu historia na jinsi mazingira yanavyoadhiri tabia za wanadamu. Katika tafiti hiyo watu 24 ambao ni wenye afya na wasio na historia yoyote ha kufanya vitendo vya kuvunja sheria waliwekwa katika jela. Baadhi walipewa majukumu ya kuwa walinzi na wengine wakawa wafungwa na kutakiwa kuishi kweli kama wafungwa na wengine kuishi kweli kama walinzi. Jaribio hilo liliwataka kila mmoja atumie nafasi yake kama anaishi kiukweli kweli na itachukua muda wa wiki mbili kumaliza utafiti huo. Lakini baada ya siku sita wale walipewa jukumu la kuwa walinzi walianza kuwaonea na kufanya ukatili kwa wenzao na kupelekea zoezi kusitishwa.
Philipo Zimbardo, ambaye ndiye aliyekuwa anasimamia zoezi lote alisema kuwa, “ Wale waliopewa nafasi ya ulinzi mwanzoni walikuwa wanafanya kama wanaigiza lakini baadaye wakawa wanafanya kweli na mpaka kuonea wenzao. Kuna waliokuwa wanawachapa kabisa wenzao, kuwapa adhabu mbaya, na kuwafanyia vitendo vibaya wafungwa."
Tafiti hiyo ilifundisha kuwa, baada ya mtu kuigiza hali fulani kwa muda mrefu inapelekea kuanza kuishi kiukweli kweli katika maigizo hayo. Hivyo utagundua kuwa leo hii unaweza ukawa unajiona ni mwema na mkamilifu lakini mazingira na mazoea madogo madogo yanaweza kubadili tabia yako bila wewe kujijua kabisa.
2. Jaribio la Kupima Uwezo wa Kutambua Badiliko la Haraka.
Utafiti mwingine maarufu katika historia uliowahi kufanyika; utafiti huo uliwagusa wanafunzi wa vyuo. Ulifanyika kwa mtafiti kumfuata mwanafunzi akiwa njiani na kumuuliza swali kisha anapita mtafiti mwingine kati kati yao akiwa amebeba ubao na wanabadilishana bila yule mwanafunzi kujua kuwa aliyekuwa anamuuliza swali amebadilika.
Utafiti huu nao ulionyesha udhaifu wa ubongo wa mwanadamu kutambua mabadiliko ya haraka. Wengi walishindwa kutambua kuwa aliyewauliza swali, na yule aliyepita kati kati akiwa amebebea mlango na kuwazuia walibadilishana.
3. Utafiti wa Stanley Milgram.
Baada ya vita vya pili vya dunia, Stanley Milgram aliamua kufanya utafiti wa kutaka kufahamu ni kwanini wanajeshi wa Nazi walikuwa wanatenda ukatili kipindi cha Utawala wa Nazi na alipenda kufahamu je Utawala wa Nazi unahusika vipi katika kuwafanya wawe wakatili.
Aliwachukua watu waliojitolea kufanya jaribio na kuwaambia wabonyeze switch ya umeme wenye nguvu kubwa kwa mwenzao. Asilima 65% ya walioambiwa walionyesha kweli kutaka kufanya hivyo lakini waliobakia walikataa kwani waliona watamuua mwenzao.
Ilionyesha kuwa mtu anaweza akafanya hata ubaya kwa sababu ameambiwa afanye na bila kufikiria madhara yake kwa wengine yeye anaweza tu kutenda alichofanya.

0 maoni:
Chapisha Maoni