Sayansi Na Dini

Posted by Unknown on 09:30 with No comments
Nicolaus Copernicus

Ni wazi kuwa kila mtu anafahamu kuwa Sayansi na Dini zimekuwa haziendani sawa na kumekuwa na utata mkubwa sana kwa wasomi wa pande zote hizi mbili. Je kipi ni sahihi? Je Dini zipo sawa na sayansi? Ni nani anampinga mwingine na yupi anapotosha na yupi yupo sahihi. Kupitia maswali haya tunaweza kukaa pamoja na kushirikiana na kuweza kufahamu kuna nini kati ya pande hizi mbili za elimu.

Sayansi.
Sayansi ni elimu ambayo mwanadamu anatumia milango yake ya ufahamu kuielewa dunia inayomzunguka. Katika sayansi tunachunguza kwa kutumia milango yetu ya ufahamu kuelewa zaidi vinavyotuzunguka. Sayansi imeanza katika maisha ya mwanadamu tangu alipoanza kutaka kuifahamu vyema dunia. Mfano mwanadamu alipoanza kutaka kujua miti ni nini? Wanyama ni nini, dunia ni nini, milima ni nini, ipoje, imeanzaje, bahari ni nini na kwanini hiki kipo hivi na kingine kipo kivingine. Hapo mwanadamu anaanza kuchunguza na kuzidi kufahamu na mpaka leo sayansi imekuwa ni sehemu kuwa ya maisha katika kuleta majibu ambayo yanapatikana kwa uchunguzi wa kutumia milango ya ufahamu wetu. Mwanadamu anapaswa kutosahau kuwa Sayansi ni sehemu ya imani, kupitia sayansi tunafahamu maajabu zaidi ya ulimwengu kuliko kushikilia kitabu cha imani na kuogopa kupoteza imani yako kwa sababu unahisi sayansi ipo tofauti. Sayansi inahitaji na inatuhamasisha kusoma, kuchunguza, kutafiti na kupata majibu zaidi badala ya kuamini tu bila uhakika wala ushahidi.

Dini.
Kupitia sayansi tutafahamu zaidi na kujua ulimwengu zaidi. Lakini bado elimu ya dini ni muhimu kwa kukuza maadili kwa mwanadamu na jinsi ya kuishi hasa katika upande ambao hatuwezi kuujua kwa milango yetu ya ufahamu. Dini kwa maana ya sasa ni taasisi inayoamini na kufuata taratibu au mfumo fulani kiimani. Katika dini ni lazima ufuate na kuamini kinachosadikika katika dini hiyo na kama huamini unakuwa umekiuka dini. Elimu ya dini inatusaidia kutupa maelekezo na majibu kwa maswali ambayo hatuwezi kupata majibu kwa kutumia milango yetu ya ufahamu lakini dini haitupatii ushahidi wa kiuhalisia katika kuchunguza zaidi.


Kihistoria.
Picha iliyochorwa kumuonyesha Galileo alipokuwa akiwaelekeza viongozi wa dini


Hapo zamani sayansi na dini vilikuwa ni kitu kimoja na vyote vilianza kutokana na nature ya mwanadamu ya kupenda kufahamu zaidi vinavyomzungua. Tangu mwanadamu kuzidi kuongeza ufahamu na kujitambua zaidi na kutambua maisha yalivyo na mazingira yanayomzunguka, kulikuwa na watu waliojitolea maisha yao kutafuta ukweli wa maisha na kufundisha watu kuhusiana na maisha. Mada kama vile milima ni nini, mabonde ni nini, mwanadamu ni nani, ametoka wapi, sayansi ya madawa ya kujitibu, uchaguaji wa chakula, mazingira yanayotuzunguka kama vile jua, nyota ni nini, n.k vyote hivi mwanadamu alikuwa anapenda kuvifahamu hivyo wale walioweza kufahamu zaidi kutokana na kutumia maisha yao kuchunguza maisha walionekana wenye busara na wakipekee. Na kwa vile ambavyo mwanadamu alikuwa haelewi alitumia Mind yake kutengeneza imagination kama vile mtu anayekaa mawinguni na wengine hata kwenye vitabu vya dini vinasema walidiriki kujenga mnara kumfikia Mungu, huu ni ushahidi jinsi mwanadamu alivyokuwa mjinga na fikra yake ilivyokuwa. Leo hii tunafahamu wasingeweza kumfikia Mungu kamwe hata kama wangetumia udongo na mawe yote ya dunia wasingemfikia kamwe. Miaka ya kale Imani ilikuwa ni sehemu moja ya Sayansi japokuwa vilikuwa duni. Vyote vilitumika kufahamu mwanadamu na wachunguzi walipewa kipaumbele cha juu kutokana na elimu zao.

Dark Ages (Kipindi cha Miaka ya Giza)
Ilipofika miaka ya Dark Ages, dini iliweza kutawala, ikaweka msingi zaidi kwenye Imani na kusahau Sayansi ambayo ilikuwa inabadilika badilika kutokana na tafiti zikizidi. Dini ilikuwa ni vigumu kubadilika kwani inaaminika kilichoandikwa tayari kimeshaandikwa hivyo hakibadilishiki. Zipo dini ambazo zilishauriwa kubadili mafundisho yake zikakataa na kupelekea hata kuchoma au kuwaadhibu wanasansi au wachunguzi. Tatizo ni kuwa vizazi vilizidi kuona kuwa Sayansi inaongopa na ni kinyume na dini. Sayansi ni kama milango yetu ya ufahamu. Mwanadamu anatumia milango ya ufahamu kama vile macho, masikio, pua, ngozi, ulimi kupata taarifa za ulimwengu wake wa nje na mazingira. Sayansi nayo ni elimu inayotegemea milango ya ufahamu kuchunguza.  Ipo miaka ambayo imani ilikuwa inaweka msimamo, haitaki kuelimika. Waliokuwa wanafundisha mambo ambayo dini haijasema walionekana wanaasi, wapo waliochomwa, wengine waliambiwa wakane kauli, na wengine walidiriki kuanzisha Temple au maeneo ya mikutano ya siri kuzungumza jinsi ya kushare elimu zao kwani walikuwa wanapingwa na jamii.

Adhabu kwa waliokuwa wanapinga dini kwa kutoa mawazo mapya.
Dhana kwamba dunia inaizunguka Jua zilikuwa hazipo na walioanzisha mada hizo walionekana ni waongo kwani watu walichukulia Maandishi ya imani kama msingi wao na elimu kuu. Japokuwa kulikuwa na madhaifu ya makanisa na dini lakini walijitahidi kukuza sayansi kwa kudhamini mashule makuu ya zamani, walisomesha wanadhiri au walimu wa kiimani waliokuwa wanapenda kusoma, mfano Galileo alikuwa na ukaribu na kanisa lakini alipokuja kusema kuwa dunia ni flat inazunguka jua na kuna sayari zina Miezi yake alionekana kaidi kwani vitabu vya imani havikuwahi kusema hivyo. Na wapo mapadre, walimu wa imani na wanafunzi waliokuja kuwa wanasansi wazuri.


Imani za Mashariki:
Mfano Hinduism na Buddhism mpaka leo zinaenda sawa katika imani na sayansi. Buddhism inaaminika ndio dini ambayo 100% inakubalika na sayansi na ni imani ambayo haikatazi ufahamu zaidi kwani sayansi na imani hiyo tangu kale vinaenda sawa na mpaka leo vinaenda sawa. Hinduism nayo imetumika na wanasansi wengi kutengeneza ubunifu mpya wa sayansi mfano ugunduzi wa umeme, Atom, Atomic Energy, Vibration, Big Bang na kadhalika vyote hivi hufahamika katika Hinduism na vimetumika na wanasayansi kuvifanya na vikaonekana ni kweli. Waanzilishi wa Nguvu ya umeme na Tesla aliyebuni Usambazaji na uzalishaji wa umeme waliandika kwenye barua zao kuwa wamesoma kwenye Hindusm na imewasaidia kubuni na kufanya tafiti zao. Concepts kama Meditation na yoga zinakubalika kisayansi, concepts za reincarnations, Cause and Effect, Nguvu ya Akili na kadhalika vyote vimeungwa mkono na sayansi. Uzuri wa imani za mashariki zinakubali kubadilika kwani zinaamini ukweli hubadilika kutokana na uwezo wa mwanadamu unavyozidi kuongezeka na pia dini haiendani mbali na sayansi.


 Dini na sayansi hapo kale vilikuwa ni kitu kimoja lakini baadaye dini zilipoanza kuwa ni kama taasisi badala ya elimu, zikawa hazipendi kubadilika kimtazamo na mwisho kupelekea kutengana. Dini zinapaswa kuwa wazi, kuruhusu watu kufanya utafiti, ziruhusu kufundisha waumini kufahamu sayansi inasema nini badaya ya kusema kuwa waumini wasisome wala kuamini sayansi kwani sayansi ni uongo wakati dini zenyewe zinanufaika na manufaa ya sanansi kama teknolojia, elimu, uchunguzi, vifaa na kadhalika. Ni kutoa fursa na kuwa wazi kubadilika kwani kubadilika hakuadhiri chochote. Ndio maana tumepewa milango ya ufahamu kuitumia na kujiweka huru kwa kuitafuta KWELI. Sayansi na dini vina lengo moja katika kutoa elimu ya kujitambua na kutambua ulimwengu vyema.

Categories: ,