Unaposhikilia Mahusiano Yanayokuumiza

Posted by Unknown on 17:42 with No comments
Kuna msemo unaosema mahusiano yaliyoharibika ni kama kioo kilichovunjika, kuna wakati inakubidi uache vipande chini kuliko kuviokota na vikakuumiza zaidi. Kila mtu anapenda kupenda na kupendwa. Na ndio maana inauma sana pale unapoumizwa au unapopenda ambapo unaona unadanganywa. Kwani kila mwanadamu anayependa anategemea kupata upendo kama alioutoa. 



Kuna wakati mahusiano yanakuwa ni magumu na yenye kukuumiza sana, mfano mwenza wako anaweza akawa anafanya kinyume na unavyopenda au anaenda kinyume na makubaliano yenu. Makubaliano kama yapi? Kukujali, kukupenda, kukuthamini, kukusikiliza na kuwepo pale unapomhitaji/anapohitajika na pia kutosalitiana. Hivi vinapokiukwa hupelekea mahusiano kuwa magumu na yenye kukuumiza kwani hivi ni SUMU ya mahusiano yoyote. 

Ni vyema kukaa na kutafakari tatizo lilipoa, kama kuna njia ya kuweza kulimaliza itumie njia hiyo na hakikisha unajitahidi kumaliza tatizo.

Inauma sana pale unaposhindwa kusuluhisha tatizo kwani mahusiano hasa ya wapenzi hupelekea muunganiko wa watu wawili na kama muunganiko huo unapotengana hupelekea maumivu kati ya watu hao wawili. Kutokana na kuzoeana sana na kufahamiana sina kunajenga muunganiko ambao unakuwa ni taabu kuuondoa. Na pale inapolazim wawili kuachana muunganiko huo ni vigumu kuuondoa kiurahisi lakini taratibu utaondoka.

Kama unaona haiwezekani kusuluhisha tatizo ni kwanini msikubaliane kuachana?

Kuna wakati inabidi uweze kutoka kwenye mahusiano na kuwa huru. Unapotoka kwenye mahusiano haimaanishi kuwa hukupenda vyema bali inamaanisha kuwa unajipenda kiasi cha kuwa hupendi kujiumiza kwa mahusiano yasiyo na umuhimu kwako. Ni vyema kuacha kushikilia hali na watu au mtu ambaye huwezi kuwa naye labda kutokana na sababu ambazo ni nje ya uwezo wako.

Kama inawezekana kusuluhisha mahusiano yanayokuumiza jitahidi usuluhishe na kama unaona haiwezekani basi achana nayo kwani itakupa nafasi ya kupata mahusiano mapya na kujiepusha na mahusiano yanayokuumiza au mahusiano yasiyo na umuhimu katika safari yako ya maisha. 

Categories: ,