Jinsi Upweke Unavyoweza Kuadhiri Maisha Yako.

Posted by Apolinary Macha on 13:00 with No comments



Upweke unaweza ukapelekea madhara makubwa hasa katika biolojia ya mwili na saikolojia. Upweke unaweza kubadili gene (DNA), kuathiri seli nyeupe na mfumo wa kinga ya mwili, ukuaji wa ubongo na neva na saikolojia kwa ujumla katika ukuaji. Katika sehemu ya ubongo upweke unapelekea mabadiliko kwenye Prefrontal Cortex (sehemu ya kortex ya mbele kabisa katika ubongo), na kupelekea matendo ya utofauti au hisia tofauti.

Tunaposema UPWEKE tunamaanisha ile hali ya kuhisi uko peke yako wakati unahitaji campan au watu wa karibu katika kushirikiana nao kwa mawazo au furaha. Kuna hali ya mtu kuwa peke yake na anaridhika nayo na hiyo sio upweke lakini pale anapoona kuna kitu kimepungukiwa na yuko peke basi hali hiyo ndiyo huleta upweke. Kuna wakati mtu huamua kukaa peke yake labda kwa kutafakati mambo mbalimbali na kukaa mbali na makelele, fujo, msongo wa mawazo na maranyingi watu wa tabia hii huitwa INTROVENTS. Hawa hupenda kuwa peke yao kurudisha energy wanayoipoteza wakiwa na watu mbalimbali, na kuna ambao wakiwa na watu na makundi mbalimbali kila siku ndio energy yao inarudi (EXTROVENTS) na kuna ambao wakiwa katika makundi ya watu na kuongea sana wanapenda baadaye wawe peke yao. Ni kutokana na kuwa mwanadamu anatofautiana kwa jinsi anavyoweza kupoteza energy yake au kuongeza energy yake.



Turudi katika adhari za upweke. Kuongezeka kwa hali ya upweke hushusha uwezo wa kinga na mwili kujitibu kwa mtu anayehisi upweke kila wakati, huongeza nafasi ya kupata magonjwa yanayohusiana na Moyo, yanayosababishwa na kushindwa kwa Prefrontal cortex mfano ADHD au Schizophrenia. 

Amini usiamini upweke hupelekea magonjwa ya moyo pia. Kutokana na utafiti wa hivi karibuni stress, msongo wa mawazo na hali ya kuhisi upweke huadhiri umeme unaotumika kusukuma misuli ya moyo katika kusukuma damu kwenye moyo.

Pia upweke hupelekea watu kufanya maamuzi mabaya kama vile kuvuta sigara kwa kuondoa msongo wa mawazo au kwa kukufanya urelax, kunywa pombe, kutumia madawa, kushirikiana na makundi mabaya kwani unahisi ukishirikiana nao utaondoa upweke wako na wengine huamua kupoteza maisha yao kwa kujiua. 

Hivyo upweke huadhiri sana maisha ya mwanadamu, anaweza akajijua au asijijue na kujikuta tayari ameshapotea kutokana na kuufuata upweke wake. 

MUHIMU SANA KUJIFUNZA KUJIDHIBITI HASA PALE MAAMUZI YASIYOSAHIHI YAKIKUFUATA NA PIA JIFUNZE KUONGOZA HISIA ZAKO NA FURAHA YAKO.

Unaweza ukajifunza kupiga kifaa cha mziki au kufanya chochote kitakachokufanya
uisahau hali ya upweke.
Ni vyema kuwa na campan, urafiki na watu mbalimbali, jifunze kuwa na furaha ukiwa peke yako kwani kama huwezi kuwa na furaha peke yako basi hata ukiwa na watu au mtu hautakuwa na furaha tu. Jifunze kufanya meditation au yoga kwani huongeza nguvu kwenye akili na ubongo, kuongeza uwezo wa mwili kwenye kinga ya magonjwa na mabadiliko ya genes. Pia tembea, jenga urafiki na watu mbalimbali unaokutana nao, jifunze kuishi vyema na watu, suluhisha matatizo ya kutoelewana na marafiki, ndugu au watu wanaokuzunguka. 

Vitu mbalimbali vya kufanya unapohisi upweke:
  • Meditation/Taamuli,
  • Yoga,
  • Kulala/Kupumzika,
  • Kusikiliza mziki,
  • Kupiga kifaa cha mziki au kujifunza kifaa cha mziki mf. Gitaa, Kinanda,
  • Kutembea,
  • Kufanya mazoezi,
  • Kwenda Beach,
  • Kutazama Movie au Maonyesho,
  • Kucheza na mnyama unayemfuga n.k