Meditation (Taamuli) na Maisha

Posted by Apolinary Macha on 14:07 with No comments

Haijalishi unajisikia hali gani au unahisi nini, kama una furaha au hauna furaha, kama una huzuni au hauna huzuni, jaribu kutafuta muda na kumeditate. Katika siku kuna mawazo ya aina mbalimbali. Kuna mawazo mengi yanakuwa yameendelea akilini, kuna hisia malimbali zilijitokeza akilini na kuna mitazamo mbalimbali imejitokeza akilini.

Tafuta wakati ukae peke yako, tuliza akili yako kwa kuiweka kwenye eneo moja au wazo moja. Unaweza ukakaa kwenye sehemu tulivu ukaweka akili yako kwenye pumzi yako huku ukiwa unaivuta na kuitoa taaratibu. Acha mawazo mbalimbali yanayotokea akilini yaendelee, weka akili yako sehemu moja na ikihama kuhamishwa na mawazo irudishe kwenye eneo moja na taaratibu mawazo yataondoka yenyewe. Utagundua kuwa wewe sio mawazo yako, wewe sio hisia zako bali wewe ni ufahamu uliopo nyuma ya mawazo, hisia na mitazamo. Wewe ni sehemu ya ufahamu inayoutazama ufahamu.

Ukiweza kutafuta muda angalau wa dakika 20 kila siku asubuhi na mapema napoamka na kabla ya kulala utaweza kuongeza faida kubwa maishani mwako na utaweza kuongeza mafanikio na furaha ya maisha. Ni elimu ambayo unaweza ukashangaa manufaa yake ni ya ajabu lakini jifunze bila kupuuzia na utakiri kuwa Meditation au Taamuli ni njia njema ya mafanikio katika maisha kwani hukuongezea umakini wa akili, busara, hekima, adabu na hukusaidia kuweza kujirekebisha kwa chochote kila unachotaka kujibadili.