Jinsi ya Kuvutia Watu Katika Maisha Yako

Posted by Apolinary Macha on 14:54 with No comments


Katika maisha mara nyingi kila mmoja anapenda kuhakikisha jamii ambayo anaishi inamjali na kumpenda. Tunapenda wazazi, ndugu, marafiki, na watu wanaotuzunguka kutusifia na kutupenda. Lakini kuna siri kuu mbili za kuhakikisha watu ambao tunaishi nao wanatupenda na kutuheshimu kama inavyostahili. Njia kuu hizi mbili zitaelezewa kwa ufupi na urahisi wa kuelewa na zinaweza kusaidia watu wengi kuweza kuishi katika maisha ambayo jamii inayotuzunguka ikatupenda na kutusifia. 

Mfano unaweza ukawa umekutana na ndugu au mtu wa jinsia tofauti na kutofahamu ni namna gani ya kuhakikisha mtu huyo anakupenda. NJia ya kupendwa ni rahisi sana na hii njia niliijua kupitia rafiki yangu aliyenipa mawazo mazuri na nitatumia blog hii kushare kile ambacho nilijifunza

Usitake Kila mtu akupende

Katika njia ya kwanza ambayo ni njia kuu inayoweza kumsaidia kila mmoja ni kuacha kutaka kumfurahisha kila mtu. Mfano unaweza ukawa umeingia kwenye basi na ukakuta watu wanakutazama na ikakupa woga wa kufurahi utakavyo. Kuna watu wa aina mbalimbali, kuna wengine wanapenda kutaka kila mgeni au mtu wanayemfahamu awasifie na kuna wengine wasiotegemea mitazamo ya  watu katika kuishi maisha yao. 

Badala ya kutaka kila mtu akusifie, anza kwanza kutotaka kila mtu akusifie. Hii ni kwasababu ni vigumu kila mtu kukusifia na haiwezekani kila mtu akakusifia katika maisha. Kuepuka kutaka kusifiwa na kila mtu au kupendwa na kila mtu kutakupa uhuru wa kuwa na furaha bila kutegemeana na mtu yoyote. Kwa maana kuwa endapo watu wakikupenda au wasipokupenda haiharibu furaha yako ya moyoni. Endapo watu wakikusifia au wasipokusifia haitaleta madhara katika furaha yako. Chunguza watu wanaopendwa na kuheshimiwa ni watu wasiopenda sifa kwa kila mtu. Cha msingi ishi na watu vizuri, heshimu kila mmoja, jali hali za watu na hisia zao na kila jidhamini na wewe binafsi bila kutaka sifa au kupendwa kwa ulazima. 

Jidhamini Kwanza

Njia ya pili kuu katika kuhakikisha unapendwa na kuheshimiwa na watu wengi ni kujithamini.. Jali maendeleo yako, kama ni kazi jitahidi kufanya kazi zako vizuri, kama ni masomo jitahidi kufanya masomo yako vyema. Pia jijengee kuwa na mwenendo mzuri katika maisha kama vile kuacha pombe, madawa ya kulevya, anasa, uchafu, na badala yake jenga mazoea ambayo yatakusaidia kuishi vyema na watu wa aina mbalimbali. 


Kwa ufupi ni kuwa, ukiweza kuishi bila kutaka sifa kwa kila mtu, na kujithamini huku ukiwa na jitihada za kuweka maisha yako vyema kila mtu anayekufahamu atakupenda na kukupa heshima yako. 

Kumbuka kuwa furaha sahihi inatoka moyoni mwako na sio kutegemeana na watu au jamii inavyokutazama.