Maneno 17 Unayoweza kujisemea Mara kwa Mara hasa Katika Wakati wa Mashaka na Wasiwasi.

Posted by Unknown on 14:29 with No comments
Kumbuka Utajiri Uliopo Ndani Mwako.
Kila siku asubuhi na jioni unaweza kusema maneno haya kabla ya kulala na baada ya kuamka. Kila usemapo matamshi haya yaseme huku ukiweka fikra zako kwenye maneno hayo na kuhisi ukamilifu wake katika maisha yako. Maneno haya kuyasema mara kwa mara itakusaidia kukumbuka thamani yako na kukaa akilini mwako na moyoni na itakukumbusha dhamani yako. Pia ni sehemu kama ya sala lakini ipo katika lengo la Kushukuru na kujikumbushia thamani yako. Unaweza ukayatamka hata kama una imani ya aina yoyote, ni kwa kila mtu ambaye anaamini safari yake ya maisha ina umuhimu na ulinzi mkubwa. 

MANENO 17 UNAYOWEZA KUJISEMEA KILA MARA NA HATA WAKATI WA SHIDA.
  1. Ninashukuru kwa kila jambo katika maisha yangu.
  2. Nina furaha kubwa ndani yangu.
  3. Nina thamani kubwa ndani yangu zaidi ya Mali zote ulimwenguni.
  4. Ninapewa kila ninachohitaji na cha umuhimu katika maisha yangu.
  5. Mimi na Mungu ni kitu kimoja naye hunilinda kwa yote tangu nilipoumbwa na hata kabla ya kuumbwa. 
  6. Ninaruhusu safari ya maisha inifundishe.
  7. Ninaruhusu uwezo wa Mungu kufanya kazi yake katika maisha yangu.
  8. Ninaamini nina malengo ya kuwepo na ndio maana nipo hapa ulimwenguni.
  9. Hakuna kinachoweza kunidhuru, kunigusa, wala kuharibu nafsi yangu ambayo ipo ndani ya mwili huu kwa sasa.
  10. Ninapendwa na ninaruhusu upendo kusambaa ndani na nje yangu. 
  11. Ninaishi katika njia sahihi ya lengo la maisha yangu.
  12. Ninaweza kutimiza kila lengo ninalolitaka.
  13. Ninamkabidhi Mungu kila kitu katika maisha yangu.
  14. Mimi ni zaidi ya huu mwili na huu muonekano. 
  15. Kila mateso na taabu za sasa ni za kupita na hazitabaki milele. 
  16. Mimi ni mzuri na nimekamilika.
  17. Ninashukuru kwa kila jambo, na ninaamini nitamaliza safari yangu katika ulimwengu huu salama na mwisho kuungana na aliye mkuu na chanzo cha vyote, Mungu mwenye Heri na Upendo wa Milele. 
Aimen.