Kuamka na Kujitambua?
Posted by Apolinary Macha on 21:30 with 1 comment
Kujitambua ni neno ambalo lipo tangu hapo kale, miaka na miaka watu
maarufu na walioweza kuona maisha katika hali tofauti tofauti wameweza
kuhimiza wengi kujitambua.
Kabla ya kufahamu kujitambua kuna msemo mmoja unaotumikaga sana unasema
"Kuamka". Katika lugha mbalimbali watu wamekuwa wakielezea kuamka.
Ukitafuta utaona katika lugha ya magharibi wanaita
"Awakening/Illumination" na katika lugha ya mashariki ni
"Enlightenment/Nirvana/Buddhahood.
Wapo wanadamu walioweza kujitambua na kuamka katika maisha. Wengine ni
viongozi wa imani kuu duniani, ni walimu wa imani, walimu wa maisha,
mifano ya kuigwa lakini wote hawa wanatufundisha kuwa mwanadamu ana
uwezo zaidi ya alio nao.
Ni vigumu sana kukuambia kuamka ni nini. Maana kuamka ni hali ya
kufahamu uhalisia wa ulimwengu, kuungana na chanzo kikuu cha ufahamu, na
kujitambua. Ni vigumu kumwambia mtu experience yake ilivyo kwani
experience haielezewi bali unatakiwa uiexperience na sio kuisikia. Ni
sawa na mtu akikuelezea Los Angeles ilivyo wakati wewe hujawahi kufika.
Utajikuta unatengeneza picha ndani ya akili yako, na huenda ukawa
unatengeneza picha tofauti kabisa na uhalisia. Ni sawa na kumuelezea
kipofu rangi nyekundu ni nini wakati hajawahi kuona rangi.
Yesu, Manabii, wote wamefundisha mwanadamu kuangalia ndani yake na
kufahamu utajiri alio nao. Ni dhahiri kuwa wanadamu wengi hasa wa imani
duni huwaamini wanadamu walioamka ni Miungu/Manabii/Walimu wao. Lakini
hata wewe na mimi tunaweza kuamka na kuwa sawa na wao. Wanayo siri kubwa
ndani na ndio maana wanatufundisha sana kujitambua na kubadilika kwa
kufuata njia sahihi za maisha. Njia hizo hatuzifuati kwa sababu ya
kwenda mbunguni au mahala ambapo ni salama baada ya maisha haya, bali
njia hizo ni asili yetu. Ni sawa na mtu aliyewahi kutembea akapooza na
sasa amepona na anajifunza kutembea tena. Unapotenda mema haumtendei
Mungu bali unajitendea wewe, kwani asili yako wewe ni utakatifu lakini
upo katika dunia ya kifizikia. Dunia ya mwili. Dunia ya milango ya
ufahamu.
Kuamka kumechorwa kama nyoka akizunguka fimbo (Uti wa Mgongo). |
Musa na Nyoka wa Shaba ambaye aliamtengeneza kutibu wana wa Israel. |
MFANO WA MWISHO:
Je una habari kuwa kila seli yako imebeba taarifa yako? Katika seli yako moja kuna information za mwili wako wote? Mwanadamu ni sehemu ya ulimwengu. Kama seli zinavyobeba taarifa ya mwili wako, wewe unabeba uasili wa muumba wako. Ukijitambua na kuamka unarudi katika asili yako. Unafunuliwa na kufahamu ulimwengu halisi na ulimwengu wa ndoto.
Lakini kuamka huko ni mpaka ujitambua, kwani print ya kuamka ipo ndani mwako.
Kuelewa kuamka ni kujitambua. Unaamka kwa kutambua kuwa ndoto ni nini na
uhalisia ni nini. Ni wazi kuwa inafahamika kuwa mwanadamu amelala,
hatambui nguvu aliyonayo na hata sayansi inasema mwanadamu anatumia
asilimia 7% tu ya uwezo wake wa ufahamu hivyo ana ufahamu mkubwa zaidi
ya alionao lakini hautumii.
SHUKRANI KWA DARASA .NI MEFAIDIKA SANA
JibuFuta