Ondoa Vipingamizi vya Kufikia Malengo Yako.

Posted by Apolinary Macha on 12:56 with 2 comments


Anza kusema HAPANA kwa vitu ambavyo vinakuzuia kufikia malengo na ndoto zako za maisha. Matendo yanayokupotezea muda wako, marafiki wabaya, watu ambao maisha yao yanaweza kukupeleka pabaya, stress, hofu, matendo yanayomchukiza Muumba na nafsi yako. Tena unachopaswa kutenda, ishi unavyopaswa kuishi na tafakari kiusahihi kila wakati. Kama unapaswa kulipa deni, na kuna mazingira yanayokuzuia kutunza kipato chako kwa matumizi mabaya, acha. Kama unapenda ueshimiwe ishi kiustaarabu na heshimu na wengine. Kama unataka usome na ufaulu kwa maksi nzuri basi ondoa uvivu, matumizi mabaya ya wakati, soma kwa bidii na fanya unalopaswa kufanya ili ufanikiwe mpango wako.

Utakapoanza kujitambua zaidi utagundua; kama unataka ufanikiwe katika maisha angalia waliofanikiwa wanaishi vipi na ishi hivyo. Kama wanaamka mapema na kusoma au kujituma katika kazi, nawe fuata utaratibu huo, jitume, stay motivated, visuallize it, dream it, never get tired to work hard on it. You will REACH there. You will find yourself there.

Belive me…